MKOPO WA CHAP CHAP

Mkopo wetu wa chap chap unalenga watu wenye uhitaji wa fedha za dharura ambao hawahitaji kusubiria muda na wala hawahitaji kufuata mchakato mrefu wa ukopaji mfano wa dharura ni kifo, ugonjwa, kesi, ajali, majanga, ada n.k.Wenye uhitaji wa haraka/dharura unaleta dhamana yako ofisini kwetu yenye thamani mara tatu ya kiwango cha mkopo unachohitaji na kupatiwa mkopo papo hapo baada ya tathimini. Kiasi cha mkopo kinaanzia Tshs 100,000/- mpaka Tshs 5,000,000/- kutegemeana na thamani ya dhamana yako. Afisa mkopo atatathimini dhamana yako na kushauriana dhidi ya kiwango unachohitaji.

Vigezo na mahitaji ya mkopo Wa chap chap

  1. Nakala ya kitambulisho cha kura,Taifa,hati ya kusafiria au leseni ya gari ya mkopajii
  2. Nakala ya kitambulisho cha kura,taifa,hati ya kusafiria au leseni ya gari ya mkopaji, mtoa ridhaa
  3. Picha mbili za passport size za rangi -Mkopaji
  4. Picha mbili za passport size za rangi -Mtoa ridhaa
  5. Barua ya utambulisho/uthibitisho wa makaazi kutoka serikali za mitaa
  6. Maekekezo mengine utakayopewa