MKOPO WA WAKULIMA

Mkopo wetu wa wakulima unalenga wakulima wajasiriamali ambao wana uhitaji wa kifedha na wamekwama katika hatua za kilimo mfano kupalilia au kuvunia au kupukuchua au kusomba mazao kutoka shambani. Kiasi cha mkopo kinaanzia Tshs 100,000/- mpaka Tshs 1,000,000/- kutegemeana na mahitaji na ukubwa wa shamba na wingi wa mazao. Afisa mkopo atakutembelea na kufanya tathmini ya shamba kuona mazao na hatua inayoombewa fedha na kushauriana dhidi ya kiwango unachohitaji.

Vigezo na mahitaji ya mkopo wa wakulima

  1. Nakala ya kitambulisho cha kura,Taifa cha mkopaji
  2. Picha mbili za passport size za rangi -Mkopaji
  3. Nakala ya kitambulisho cha kura,taifa cha mtoa ridhaa na mdhamini mmoja
  4. Picha mbili za passport size za rangi -Mtoa ridhaa na Mdhamini
  5. Barua ya utambulisho/uthibitisho wa makaazi kutoka serikali za mitaa
  6. Maekekezo mengine utakayopewa